Mchezaji Bacca Awaomba Radhi Yanga

Bacca awaomba radhi Yanga


Kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa beki wa kati Ibrahim Bacca dakika ya 21 tu, imeiponza Yanga kupoteza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu huu mbele ya Azam FC na kutibuliwa rekodi mbalimbali ilizokuwa nazo msimu huu ikiwamo kupoteza uwanja wa nyumbani tangu msimu uliopita.


Yanga iliyokuwa imecheza mechi zaidi ya 50 nyumbani na pia kucheza mechi nane mfululizo za Ligi Kuu msimu huu bila kupoteza wala kuruhusu bao lolote, lakini bao la dakika ya 34 la Gibril Sillah lilitibua kila kitu kwa kocha Miguel Gamondi kwa Azam kuendelea pale ilipoishia msimu uliopita ilipoichapa Yanga 2-1.


Katika mchezo huo uliopigwa kuanzia saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Yanga licha ya kupambana kiume kutaka kulinda heshima iliyonayo, ilijikuta katika wakati mgumu mbele ya Wanalambalamba walioamua kutumia mtindo wa kubaki basi hasa kipindi cha pili.


KADI YA BACCA


Mapema tu Yanga ilikumbana na pigo baada ya beki wake Ibrahim Hamad 'Bacca' kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 21 kufuatia beki huyo kumuangusha mshambuliaji wa Azamm Nassoro Saadun wakati akielekea kufunga. Mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara ambaye anashikilia tuzo ya mwamuzi bora wa msimu uliopita alisimama imara akimtoa nje Bacca, beki huyo akiifanya timu yake kucheza pungufu.


BACCA AOMBA RADHI


Wakati mashabiki wa Yanga wakichanganyikiwa na kadi hiyo nyekundu, Bacca mwenyewe aliwaomba radhi mashabiki wa timu yake wakati akitoka nje kuelekea vyumbani huku nao wakimpigia makofi wakiwa na huzuni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad