Meneja Uwanja wa Chamazi Complex Matatani Kisa Yanga...Popat awa Mbogo




Baada ya YANGA kususia uwanja wa Azam Complex, na kutangaza kuhamia uwanja wa KMC Complex. CEO wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat' aliita kikao cha dharula kwa wafanyakazi wote wa uwanja wa chamazi na kufanya kikao kizito chenye lengo la kujua hasa nini chanzo cha mteja wao YANGA Kuondoka.

Kabla ya kikao hicho uchunguzi alioufanya POPAT Iligundulika kuwa zile video za kwenye CCTV ilikuwa ni mpango wa kutengeneza na wahusika wakuu ni wafanyakazi wa Uwanja wa Azam Complex akiwemo pia Meneja wa Uwanja huo.

Jamaa kawekwa kitimoto aeleze kitu ambacho kimetokea baada ya matukio ya CCTV Camera za uwanja huo kuvuja na kwanini vitendo vile vinatokea katika uwanja huo. Meneja alijitetea kuwa video zile hazikuwa serious na lilikua kama jambo la utani tu lakini mwisho wa siku limeleta taharuki kwa mabosi hao.

Popat amemtaka ajitathmini, Aondoke au abaki na kama anabaki basi analipwa vipi? wakati wateja wakuu wa Uwanja huo wameondoka? Mishahara ya wafanakazi wa uwanja italipwa kwa pesa gani?

Tutegemee lolote siku mbili hizi.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad