Mkataba wa Kuhudhurua Sherehe za Diddy Wawekwa Wazi
Mkataba wa kuhudhuria sherehe za Diddy umechapishwa na TMZ, ukionyesha masharti magumu, yanayowataka wahudhuriaji kuficha taarifa zote kuhusu sherehe hizo.
Wahudhuriaji wa sherehe za Diddy walilazimika kusaini mkataba wa kutofichua (Non-Disclosure Agreement) unaowazuia kuelezea habari yoyote kuhusu Diddy, familia yake, marafiki, washirika wa biashara, au wapenzi wake wa zamani na wa sasa.
Mkataba huu unakataza wageni kupiga picha au kurekodi video kwenye tukio hilo bila ruhusa iliyoandikwa na Diddy. Hii inajumuisha kushea picha au video kwenye mitandao ya kijamii.
Wageni hawaruhusiwi kufanya mahojiano, kuandika vitabu, au kutoa habari yoyote kuhusu Diddy au sherehe zake bila idhini ya maandishi yaliyoidhinishwa na Diddy.
Mkataba huu unadumu kwa muda wa maisha yote ya Diddy au kwa jumla ya miaka 70, kipindi kinachotajwa kuwa muda mrefu zaidi kwa NDA yoyote.