Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko amekanusha taarifa zilizozua taharuki mitandaoni kwamba Shule ya Msingi ya Ubungo National Housing ambayo ni ya Serikali, imeuzwa kwa Wawekezaji.
Akiongea jana November 13,2024 kwenye mahojiano maalum DC Bomboko amesema Shule hiyo haiuzwi na wala hakuna mpango wa kuiuza.
Ameeleza zaidi kuwa upo mpango wa kuipandisha hadhi Shule hiyo kuwa English Medium hivyo amewataka Wazazi kutokuwa na hofu kwamba hata ikipandishwa hadhi Watoto wanaosoma Shuleni hapo watapewa kipaumbele na hakuna atakayehamishwa.
“Shule hii ina Watoto 600 ni Mtu Mjinga au Mpumbavu anaweza kufikiria Watoto 600 Serikali inaweza kuwatelekeza kwa kuuza Shule ambayo ni mali ya Umma au mali ya Serikali, kuna madarasa mapya manne, hatuwezi kuwa na mpango wa kuuza Shule halafu tunaendelea kujenga madarasa” ——— DC Bomboko.