Mrembo Afariki Dunia Akifanyiwa Sajari ya Pua...



Binti wa Miaka 22 Afariki Dunia akiwa kwenye Kitanda cha Upasuaji wakati akifanyiwa Surgery ya Pua na daktari aliyempata kwenye mitandao ya kijamii (TIKTOK) nchini Italia.

#MargaretSpada, mwenye umri wa miaka 22 kutoka Lentini huko Sicily, alisafiri hadi Clinic ambayo haikutajwa jina huko Roma kwa ajili ya kufanyiwa Surgery ya Pua mnamo Novemba 4 baada ya kuona tangazo la kituo hicho kwenye TikTok.

Lakini alidhoofika muda mfupi baada ya kupewa ganzi na akapoteza fahamu kabla ya upasuaji wa rhinoplasty kuanza.Majaribio mengi ya kumfufua #Margaret yalifanyika lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi na alikimbizwa hospitalini.

Siku tatu baadaye, #Margaret alifariki akiwa kitandani katika hospitali ya Sant'Eugenio huko Roma, kulingana na La Repubblica.

Katika hali ya kuhuzunisha, mpenzi wa Margaret, ambaye alikuwa katika eneo la kusubiri hali yake ilipozidi kuwa mbaya, alipelekwa katika chumba cha upasuaji ili kumuona mpenzi wake alipokuwa amepoteza fahamu.

Akiwa ameshtushwa na tukio hilo, aliamua kupiga picha fupi ya kile kilichotokea katika chumba cha upasuaji - picha ambazo sasa zinakaguliwa na wachunguzi kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji, kulingana na La Sicilia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad