Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kitaifa la uchunguzi wa Fedha wa Equatorial Guinea, Baltasar Engonga, amekamatwa.
Bw. Baltasar alikamatwa kwa madai ya kurekodi video chafu zaidi ya 400, akiwa na wake za watu mashuhuri nchini humo.
Kashfa hiyo iliibuka wakati wa uchunguzi tofauti kuhusu madai ya ulaghai dhidi ya mzee huyo wa miaka 54, wakati mamlaka ilipofichua daftari la CD zilizokuwa na maandishi machafu wakati wa upekuzi nyumbani kwake na ofisini.
Miongoni mwa watu waliohusishwa na rekodi hizo ni wenzi wa viongozi wa ngazi za juu, akiwemo mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Polisi, wanafamilia wa karibu na ndugu wa viongozi wakuu serikalini, akiwemo dadake Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo na wenzi wa Mawaziri.
Rekodi hizo ziliripotiwa kuwa za maafikiano lakini zimevuja mtandaoni, na kusababisha ghadhabu kubwa ya umma na uchunguzi mkali kutoka kwa vyombo vya habari vya ndani.