Unaambiwa sasa kiwango cha Mudathiri Yahya kipindi hiki ni mara mbili ya kipindi akiwa mbichi kabisa, inashangaza sana 😅, Mudathiri katika michezo mikubwa amekua akifanya maamuzi makubwa na yasiyotegemewa, katika timu ya Taifa Mudathiri Yahya amemuweka benchi mara nyingi mchezaji anayetoka ligi ya nje na aksubiri kushuhudia kazi kubwa ya mchezaji anayecheza ligi ya ndani,
Jambo la kushangaza zaidi unaambiwa Mudathiri alieahi kuachana na soka na kwenda kwao Zanzibar kuendelea na shughuli zake, punde si punde makachero wa pale jangwani wakamuona na haraka sana kuelekea taatifa kwa mabosi, mabosi bila kuchelewa wakamleta jangwani,
Timu ya Taifa inapaswa kuishukuru Yanga kwa kuweza kumfufua tena Mudathiri kutoka mavumbini mpaka sasa yupo juu mawinguni huku mchango wake mkubwa wa kukusaidia timu ya Taifa kufuzu Afcon ukioneka,
Kinachoshangaza zaidi Mudathiri Yahya kadri umri unavyozidi kwenda ndiyo anazidi kuwa wa moto sana, unaweza kufikiri ni kijana wa miaka 24.