Musonda wa Yanga Ndo Huyu Huyu wa Timu ya Taifa ya Zambia?

Musonda wa Yanga Ndo Huyu Huyu wa Timu ya Taifa ya Zambia?


Utajiuliza. Kennedy Musonda huyu wa Yanga ndiye Kennedy Musonda wa Chipolopolo? Ama wa Jangwani siyo huyu wa Zambia? Maana yule wa Zambia ni balaa zaidi ya huyu wa Yanga?


Mpaka sasa ndiye mchezaji pekee aliyeiwakilisha Ligi Kuu Bara kwa kishindo. Akionesha ubora mkubwa akiwa na kikosi cha Zambia, katika mechi za kufuzu Afcon 2025 huko Morocco.


Usiku wa Jumanne Novemba 19, 2024. Baada ya kuisha mechi za kufuzu Afcon. Kennedy Musonda alikuwa kaweka kambani goli 4. AkiMpiku hata Sadio Mane wa Senegal mwenye goli 3.


Wakati akiweka goli mbili dhidi ya Sierra Leone, Ivory Coast na Chad. Zambia ilifuzu Afcon ikiwa na goli 7. Kudhihirisha kwamba Musonda kafanya kazi kubwa kuipeleka timu yake Afcon.


Musonda yupo nafasi ya 3, kwa vinara wa ufungaji kwenye mechi za kufuzu Afcon. Akiwa sawa na Amine Gouiri wa Algeria, ambaye anakipiga kwenye klabu ya Rennes ya Ufaransa.


Pia yupo mshambuliaji wa Misri, Mahmoud Ahmed Ibrahim maarufu kwa jina la Trezeguet. Youssef En-Nesyri staa wa taifa la Morocco na klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki.


Yupo pia Sadio Mane wa Senegal na Al Nassr ya Saudi Arabia. Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon. Na Victor Osimhen wa Niageria na Mohamed Salah wa Misri.


Musonda anapatwa na nini akiwa Yanga? Au ndo kutafuta namba kwa kocha jipya Saed Ramovic? Ama shida alikuwa Master Miguel Gamond? Musonda wa Zambia ni shida nyingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad