Rais Guinea Ateua Mrithi wa Baltasar Aliefanya Mapenzi na Wanawake 400

 

Rais Guinea ateua mrithi wa Baltasar aliefanya mapenzi na Wanawake 400

Rais wa Guinea Ikweta, Obiang Nguema Mbasogo amemteua Zenon Avomo kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF).


Zenon anachukua nafasi hiyo baada ya mtangulizi wake, Baltasar Engonga, kuondolewa kufuatia kashfa ya madai ya ukiukaji wa maadili katika ofisi ya umma.


Kashfa hiyo ilifichuka baada ya uchunguzi kugundua video zaidi ya 400 zilizorekodiwa katika ofisi ya Engonga, zikiwemo video zinazowaonyesha wake na jamaa zake na maofisa wakuu serikalini, wakiwemo mawaziri na maofisa wa polisi, katika mazingira ya utata.


Kusamba video hizo kumeleta wasiwasi mkubwa ndani ya serikali na kuanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa waliohusika.


Katika hatua thabiti ya kuimarisha uadilifu katika ofisi za serikali, Serikali ya Guinea Ikweta imeagiza kufungwa kwa kamera za ulinzi katika taasisi zote za umma. Hatua hii inalenga kufuatilia tabia ya maofisa kwa karibu zaidi, kuzuia mwenendo usiofaa, na kurejesha imani kwa wananchi katika ofisi za umma.


Zenón anatarajiwa kutumia uzoefu wake katika nafasi yake mpya ANIF. Akiwa na taaluma katika sheria na fedha. Pia ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Equatorial Guinea na ameshika nafasi mbalimbali za juu, ikiwemo Jaji wa Mahakama ya Malabo, Mkurugenzi Mkuu wa Masomo ya Mikataba na Masoko ya Serikali katika Wizara ya Fedha, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Madini, Viwanda, na Nishati.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad