Rais na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mavin Records hadharani

 

Marvin

Mmiliki wa studio ya muziki, Don Jazzy amemtangaza Tega Oghenejobo kuwa ndiye Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shughuli za Mavin Records ambayo sasa inaitwa Mavin Global.


Jazzy amefurahishwa na kujitolea kwa Tega katika kusaka vipaji, ambavyo imesaidia Mavin Records kufika kimataifa.


“Ninajivunia kutangaza nafasi iliyochukuliwa na Tega kama Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shughuli zote za Mavin. Watu mara nyingi hunipongeza kwa kugundua vipaji vya wengi lakini mafanikio yote hayo yanatokana na uvumilivu wa Tega,” amesema Don Jazzy.


“Tangu siku za awali, nimemwona akionyesha udadisi kuhusu biashara, akijenga timu, akikuza watendaji na kuunda kazi endelevu kwa vipaji vyetu. Kujitolea kwake katika kuikuza Mavin na kuendeleza muziki wa Kiafrika, hakuyumbayumba na kwa pamoja tutaendelea kuunda msingi mpya kwa wasanii wetu” amesema Jazzy.


Mavin Records, sasa Mavin Global, pia walimpongeza Tega, wakisema, “Tuna furaha kumtangaza Tega Oghenejobo kama Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shughuli za Mavin Global. Jukumu hili lililopanuliwa linaangazia michango muhimu ya Tega na jukumu lake katika mustakabali wetu wa kimkakati.


Tega akiingia katika nafasi yake mpya, Mavin itaendelea kukuza ushawishi wake duniani, kuinua vipaji vya kipekee na kuweka viwango vipya vya wasanii wetu.


Alipokubali kupandishwa cheo, Tega alimshukuru Don Jazzy, akisema: “Ni heshima kuchukua jukumu hili kama Rais na Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Mavin. Asante, Kiongozi Mkuu @donjazzy, kwa imani yako, uongozi wenye maono na kuniamini kusaidia kutekeleza dhamira yetu na timu ya Mavin na ndani ya tasnia kwa ujumla.


“Asante kwa uzoefu wenu umepanua mtazamo wangu na kuniwezesha kuongoza kwa malengo. Kwa pamoja, tutaendelea kuvuka mipaka, kuwatia moyo wengine na kuacha athari ya kudumu kwa mustakabali wa Mavin Records,” aliandika.


Mavin Records inasimamia wasanii akiwemo Rema, Ayra Starr, Crayon, Johnny Drille, Ladipoe, Magixx, Boy Spyce, Bayanni na Lifesize Teddy wengine ni Don Jazzy mwenyewe, Altims, London, Baby Fresh na Andre Vibez huku kwa mwaka huu wakiwa wamemuongeza DJ Big N kama DJ rasmi wa lebo hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad