Rais Samia Aagiza Kuhojiwa Kwa Mmiliki wa Jengo Lililoporomoka

Rais Samia Aagiza Kuhojiwa Kwa Mmiliki wa Jengo Lililoporomoka

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu baada ya zoezi la uokoaji kukamilika Kariakoo, aongoze Timu ya Wakaguzi waendelee na zoezi la kukagua eneo lote Kariakoo ili kupata taarifa ya hali ya majengo pia Polisi wamuhoji Mmiliki wa jengo lililoporomoka.

Akihutubia Taifa kutoka Nchini Brazil leo November 17,2024, Rais Samia amesema “Ndugu Wananchi nimesema kuwa kipaumbele chetu kilikuwa ni kuokoa Wananchi wenzetu kwanza, baada ya zoezi hili kukamilika namtaka Waziri Mkuu aongoze timu ya Wakaguzi waendelee na zoezi la kukagua eneo lote la Kariakoo na tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya Kariakoo ilivyo”


“Kwa upande mwingine Jeshi la Polisi nalo lipate taarifa kamili kwa Mmiliki wa jengo lililoporomoka jinsi ya ujenzi ulivyokuwa ukifanyika”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad