Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza Jumatano, Novemba 27, 2024, kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa ili kuwawezesha wananchi wote kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Tamko hili limetolewa kwa mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, na lina lengo la kuhakikisha kila mwenye sifa ya kupiga kura anatumia haki yake bila vikwazo. Tangazo hili limewekewa Lakiri ya Umma tarehe 22 Novemba 2024, jijini Dodoma.