“Basi wito wangu kila mmoja atimize wajibu wake kikamilifu, ukiangalia jengo hili lilivyojengwa bila shaka lilipata vibali kutoka taasisi ya serikali halmashauri.
“Kibali jambo moja usimamizi jambo jingine jengo halikutazamwa ubora wake wakati wa ujenzi, niwaombe watu wote tunaohusika kwenye mambo haya Serikali Kuu, Halmashauri, viongozi wa serikali za mitaa asasi za kiaraia na wananchi wote kwa ujumla tuseme kwa pamoja kwamba matukio ya aina hii yasijirudie kwasabu tukio hili ni huzuni kubwa sana kwa taifa letu”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi alipotembelea katika eneo lililoporomoka jengo la ghorofa Kariakoo, Dar es Salaam.