Serikali: Mmiliki Mmoja wa Jengo Lililoanguka Kariakoo Amekamatwa

Serikali: Mmiliki Mmoja wa Jengo Lililoanguka Kariakoo Amekamatwa


Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba amesema Wamiliki wa jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo tayari wanajulikana na mmoja wao ameshakamatwa ambapo amewataka Wananchi wawe na amani na waiachie Serikali ifanye kazi yake bila kuvuruga uchunguzi na kuahidi kuwa uchunguzi ukikamilika taarifa itatolewa.

Akiongea leo November 26,2024 akiwa Kariakoo Makoba amesema “Mwenye jengo hili hawezi kukosa kujulikana, tunamjua na mmoja wao ameshatiwa nguvuni (ameshakamatwa) kwa kwasababu ni suala la kiuchunguzi Polisi wakiwa tayari watatoa taarifa ili tusiharibu uchunguzi, na niwahakikishie tu Watanzania Serikali haiwezi kushindwa kwahiyo tuwe na amani na majibu yatapatikana”

“Tume iliyoundwa, kamati ya uchunguzi imeshaanza kazi, hata kabla hamjaja hapa wengine walikuwa wanachukua sampuli ya baadhi ya vitu vilivyotumika katika ujenzi na wenyewe wakiwa tayari watatuambia tusiharibu uchunguzi”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad