Simba na Yanga Kupanda Ndege Moja Kwenda Algeria



SERIKALI imesema inaangalia uwezakano wa kuwapa Simba na Yanga ndege moja kwa ajili ya kwenda nchini Algeria katika michezo yao ya Kimataifa ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga wanakwenda kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger, Desemba 7 huku Simba ikitarajiwa kucheza Desemba 8, mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine FC.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema wamepokea wazo la wadau na kufanyia kazi suala hilo ili ikiwezekana wapate ‘Air Bus’, moja ambayo inaweza kusafirisha timu mbili na baadhi ya mashabiki.

“Tumeridhishwa na viwango vya hizi timu katika michuano ya Kimataifa, Yanga walifungwa mechi ya kwanza na Simba ilifanya vizuri zote zilicheza nyumbani.

Tunaimani makocha wa timu hizo wanafanyia kazi mapungufu ya vikosi vyao na kujiandaa na michezo ijayo wanayokwenda kucheza nchini Algeria,” amesema.

Msigwa amesema usafiri wa Algeria ni mgumu , Simba na Yanga zinaenda kuwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa ni jambo la nchi hivyo watalazimika kupanda ndege moja, kuelekea nchini humo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad