Simon Msuva Awa Lulu Baada ya Kuipeleka Taifa Stars AFCON, Dili Jipya Lanukia

 

Simon Msuva Awa Lulu Baada ya Kuipeleka Taifa Stars AFCON, Dili Jipya Lanukia

DURU za usajili zinasema Simon Msuva anasubiri ofa ya mkataba mpya wa miaka miwili na klabu yake ya Al-Talaba SC ya Irak kwani ule wa sasa umalizika mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema mabosi wa Al-Talaba wameanza kumshawishi Msuva kuendelea kuitumikia timu hiyo kutokana na mchango wake mkubwa tangu alipojiunga nao.

Msuva ambaye mpaka sasa ameifungia timu mabao mawili na kutoa asisti moja kwenye Ligi Kuu Irak ameanza kuzivutia klabu kadhaa za ligi hiyo, jambo linalozua hofu kwa Al-Talaba kwamba huenda akachukuliwa na wapinzani.

Kwa mujibu wa ripoti, moja ya klabu zinazotajwa kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ni Naft Al-Basra SC, ambayo imeweka wazi mipango ya kufanya maboresho kwenye kikosi chao katika dirisha dogo la usajili.

Hata hivyo, Msuva, ambaye ametoka kuivusha Taifa Stars kufuzu kwa mara ya nne kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), amesema bado hajapokea taarifa rasmi kuhusu mkataba huo mpya lakini ameonyesha kufurahia kutambuliwa kwa kazi yake.

“Sijapata taarifa rasmi kuhusu hilo, lakini ni jambo zuri kuona watu wanaanza kuthamini kile ninachofanya. Hii inanipa motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi,” alisema Msuva.

Msuva amekuwa mhimili muhimu kwa Al-Talaba SC, akionyesha kasi, maarifa, na nidhamu ambayo imekuwa ikiwapa ushindi muhimu kwenye michezo yao. Hali hiyo imemfanya kuwa mchezaji wa kuaminika na kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.

Kwa sasa, mashabiki wa Al-Talaba SC wanasubiri kwa hamu kuona iwapo klabu hiyo itafanikiwa kumbakiza Msuva, huku klabu nyingine zikiendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa mchezaji huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad