Waziri Mchengerwa amesema amechukua hatua hiyo kufuatia maoni mbalimbali waliyoyapokea kutoka kwa Wadau wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa vikiwemo Vyama vya siasa kuhusu mchakato wa uteuzi na ushughulikiaji wa pingamizi za Wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muda wa kuwasilisha na kutoa maamuzi ya rufaa za wagombea ambao hawakuteuliwa,.
“Ninazielekeza kamati za rufani za Wilaya kuitisha fomu za Wagombea wote walioenguliwa/hawakuteuliwa ili kufanya mapitio na kujiridhisha na sababu zilizopelekea Wagombea hao kutoteuliwa ili haki iweze kutendeka kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi, ninawaelekeza Wasimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri zote kuwarejesha
Wagombea wa Vyama vyote ambao walienguliwa kwa sababu ya kutodhaminiwa na Vyama vyao katika ngazi ya Kijiji/Mtaa pamoja na kuwa Vyama hivyo viliwasilisha barua za kuainisha gazi ya chini ya udhamni kuwa ni Kata ikiwemo Chama chanACT-Wazalendo kilichowasilisha ngazi yake ya udhamini kuwa ni ngazi ya Kata”
“Ninavihimiza Vyama vya siasa ambavyo Wagombea wao wameenguliwa kutumia vizuri muda huu wa siku mbili ulioongezwa endapo hawakuridhika na uamuzi wa Wasimamizi wasaidizi kuhakikisha wanasimamia Wagombea wao wawezenkuwasilisha rufaa zao kwa kamati za rufani zilizopo katika kila wilaya husika”