Hatimaye amekubali mazungumzo yakafanyike kwa uongozi wa timu yake baada ya kugomea kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Azam Fc ambao mkatataba wake unaisha mwakani uongozi wa Azam Fc ulikuwa kwenye jitihada kubwa ya kupambana kumuongezea mkataba wa kuendelea kusalia katika Club hiyo fundi huyo wa mpira kutoka Zanzibar lakini hadi sasa hajasaini na kijana anataka kuondoka klabuni hapo kwenda kutafuta changamoto nyingine nje ya club hiyo.
Taarifa kutoka chanzo cha ndani cha mchezaji huyo zinasema kuwa tayari kiungo huyo fundi wa mpira amefanya maamuzi ya kwenda kujiunga na @simbasctanzania yenye maskani yake Kariakoo msimbazi Jijini Dar es Salaam dirisha hili dogo la usajili anachokisubiria ni uongozi wa Simba kumalizana na Uongozi wake wa Azam Fc ili kila kitu kiwe sawa na kama mambo yatakwenda sawa basi dirisha dogo atakuwa yupo tayari kuvaa jezi ya Msimbazi nyekundu na nyeupe.
Chanzo hicho makini na cha ndani kilichopo karibu sana na mchezaji huyo kimeendelea kubainisha kuwa kwa sasa timu pekee ambayo Feisal Salum Abdalah Fei Toto anaitaka kuichezea kwa hapa Tanzania ni Simba Sports Pekee na analiona hilo likienda kutimia hivi karibuni malengo yake kwa sasa ni kuwa mchezaji mkubwa sana anayetambulika Barani Africa na uwezo huo anao Mwenyezi Mungu akijaali basi kila kitu kitakwenda sawa.