Treni ya Mchongoko Yasimama GHAFLA, TCR Yaomba Radhi

Treni ya Mchongoko Yasimama GHAFLA, TCR Yaomba Radhi



Shirika la reli Tanzania (TRC) limeeleza kuwa kumetokea hitilafu katika mfumo wa uendeshaji wa treni ya umeme hali iliyopelekea treni ya mchongoko (EMU) iliyoanza safari Dar es Salaam kwenda Dodoma saa 2:00 asubuhi kusimama ghafla majira ya saa 2:20 kati ya pugu na soga huku hitilafu hiyo ikisababisha pia mvurugiko wa ratiba za treni hiyo siku ya leo.

Taarifa iliyotolewa na TRC imeeleza kuwa Mafundi wako eneo la tukio wanafanyia kazi changamoto hiyo.

"Shirika la reli tanzania (TRC) limeomba radhi kwa abiria wa treni ya mchongoko (EMU) walioanza safari yao Dar es Salaam kwenda Dodoma saa 2:00 asubuhi na kusimama ghafla majira ya saa 2:20 kati ya pugu na soga"

"Aidha, tunaomba radhi pia kwa abiria wetu wa treni ya saa 11:15 alfajiri kutoka dodoma na treni ya saa 3:30 kutoka dar es salaam ikijumuisha safari nyingine za siku ya leo ambazo zimeathiriwa kufuatia hitilafu kwenye mifumo yetu ya uendeshaji"

"Mafundi wetu wako eneo la tukio wanafanyia kazi changamoto hiyo, tutaendelea kuwapatia taarifa
Tunatanguliza shukurani" - imeeleza taarifa ya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad