UPDATE Mpya: Vifo Ajali ya Ghorofa Kariakoo Vyafika 29

UPDATE Mpya: Vifo Ajali ya Ghorofa Kariakoo Vyafika 29


Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, amesema idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es salaam imefikia 29 hadi kufikia leo November 26,2024 huku akisema lipo pia zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kwa kutumia teknolojia ya vinasaba(DNA) na wakishathibitisha watatoa taarifa.


Akiongea mchana huu Kariakoo, Makoba amesema “Mpaka kufikia muda huu ambao tunazungumza kwa bahati mbaya namba ya marehemu ambao tumethibitisha ni 29, kwahiyo namba imeongezeka kidogo tunaendelea kuwaombea wenzetu wapumzike kwa amani”


“Lipo zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kutumia teknolojia ya vinasaba(DNA) na wenyewe tutatoa taarifa tukishathibitisha Ndugu pamoja na miili ya wenzetu, kwa upande wa majeruhi idadi ipo palepale”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad