Upinzania Mnakosa Mikakati Imara ya Watu Kujitokeza Kugombea

Upinzania Mnakosa Mikakati Imara ya Watu Kujitokeza Kugombea



 "Wagombea wote warudishwe kama makosa ni makosa madogo madogo, lakini ninauliza swali kwa wapinzani nchi hii, je, mliweka wagombea kwenye vitongoji vyote, vijiji vyote na mitaa yote? Kuna sehemu vyama vya upinzani mnakosa mikakati na mipango imara ya kuwapa watu fursa za kujitokeza kugombea, zipo wilaya hamna hata ofisi za chama na wananchi hawajui hata barua za chama wakachukulie wapi. Niliwahi kushauri sana, upinzani nendeni mkawekeze vijijjni ili wananchi watambue uwepo wenu mkanipuuza na wengine kutukana, sasa ngoja takwimu zije sidhani kama hata nusu wagombea nchi nzima mmefanikiwa kuwaweka katika kila kijiji na vitongoji. Msiende tena kwenye uchaguzi mwakani na udhaifu huu, mkubali kukosolewa, wekeni mikakati ya kujenga mtandao wa vyama vyenu vijijini".


"Ninawashangaa sana CCM na TAMISEMI, sijui wanahangaika kuengua wapinzani, Kwanini? Kwasababu hata bila kuenguliwa najua CCM itabaki yenyewe kwenye vitongoji na vijiji vingi tu, wananchi bado hawapati fursa ya vyama vingi huko vijijini, bado mtandao wa mfumo wa vyama vingi sehemu nyingi bado changamoto. Mfano, Ngorongoro tu yenye vijiji karibu 70, wote kwa pamoja CHADEMA na ACT Wazalendo hawajafikisha wagombea wa vijiji 30, vitongoji na kwenye kamati za vijiji ndio hamna kabisa, sasa hii ndiyo picha halisi ya maeneo mengine. Wapinzani tafuteni wasukaji wa mikakati na mfanye kazi kama timu ndiyo mtafanikiwa. Nchi hii ni kubwa sana bila mikakati 'hamtoboi' na mtakuwa mnawanyima fursa Watanzania wa vijijini kushiriki mfumo wa kikatiba vya vyama vingi. Na mbaya zaidi mtu hawezi gombea hadi awe na chama , kwahiyo tunavunja haki za wananchi kwa kuwalazimisha wagombee kwa vyama wakati huko vijijini vyama havipo. Hoja ya mgombea binafsi ingesaidia sana kuongeza idadi ya wagombea hasa yale maeneo ambayo vyama havijafika"- Olengurumwa.


Andiko la Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa katika ukurasa wake wa mtandao wa X kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini Tanzania.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad