Wimbo mpya wa Maua Sama uitwao 'Kariakoo', aliouachia hivi karibuni kwa kushirikiana na @Ibraah_tz, @Jaivah, na @GnakoWaraWara, umekumbwa na changamoto baada ya kuondolewa kwenye mtandao wa YouTube kufuatia malalamiko ya ukiukwaji wa hakimiliki. Wimbo huo, ambao ulitolewa Jumatano, ulikuwa umeanza kupata umaarufu kwa kasi na kufanikiwa kuingia katika orodha ya nyimbo zinazotrend, ukichukua nafasi za juu ndani ya masaa 24 ya kwanza.
Kwa mujibu wa @mackmwinshaha, Meneja wa @MauaSama, tayari mhusika aliyeripoti hakimiliki ameweza kupatikana, na juhudi za kurejesha wimbo huo zimeshaanza. Mack alifafanua kuwa kuondolewa kwa wimbo huo hakuhusiani na lebo ya @WCB_Wasafi, ambapo @IamLavalava, msanii wa WCB, pia kuachia wimbo wenye jina #Kariakoo siku hiyohiyo.
Hali hii imekuwa ya kawaida kwenye YouTube, ambapo mara nyingi video huondolewa haraka pindi inaporipotiwa, hata kabla ya kusikiliza upande wa pili. Mashabiki wa Maua Sama wana matumaini kuwa wimbo huo utarejeshwa haraka ili waendelee kufurahia kazi mpya ya msanii wao. ✍️: @enkyfrank