Christina Mwagala Afisa Habari wa Tabora United amesema ikiwa Yanga SC haijaridhishwa na matokeo ya jana waombe mechi irudiwe.
“Kama Yanga wanaona wameonewa waandike barua bodi ya ligi wabadilishiwe hi mechi alafu wao wenyewe wachague wakitaka tukacheze Avic town
tutaenda wakitaka tukacheze juu kwenye mawingu popote pale wanapotaka wao na tutawafunga vilevile kama hawajaridhika.”
“Kwamana watu waliondoka wamenuna kwamba hawajaridhika ni wakati wao kuomba mechi irudiwe, Turudiane alafu tuwapige tena sita baada ya hizi tatu,Nyuki hakunbatiwi wala hapigwi busu” Christina Amesema