Abdul Nondo Akutwa na Kiasi Kikubwa Cha Sumu Mwilini..Hali Bado si Nzuri


Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama cha #ACTWazalendo, Abdul Nondo kutekwa na ‘Watu Wasiojulikana’, imeelezwa kuwa mwili wake umegundulika kuwa na kiasi kikubwa cha Sumu

Taarifa iliyotolewa na ACT Wazalendo imesema mbali na majeraha aliyopata, pia Madaktari wamebaini uwepo wa Sumu mwilini ambayo haijafahamika kama imetokana na athari za kupigwa na kuteswa au alipewa kitu chenye sumu na waliomteka

Aidha, taarifa hiyo imesema hali ya Nondo bado sio nzuri na anaendelea kupata matibabu na kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kubaini aina ya sumu iliyopo mwilini mwake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad