Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamsaka Mwita Yoba kwa tuhuma za kuchoma nyumba na kusababisha vifo vya Watu wanne akiwemo Mama na Watoto wake watatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi amesema tukio hilo limetokea December 30, 2024 katika Kitongoji cha Kwedichocho, Kijiji cha Manga, Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Amesema waliofariki ni Pili Saguge (28), Mkulima na Mkazi wa Kwedichocho (Mama), Chacha Nyabilenga, Jane Nyabilenga na Makabala Nyabilenga ambapo Mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda Mchunguzi amesema chanzo ni Mtuhumiwa kuishutumu Familia hiyo kwa madai ya kumuua Mtoto wake kwa sumu, hali iliyomsukuma kutekeleza mauaji hayo kwa nia ya kulipiza kisasi.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linatoa wito kwa yoyote mwenye taarifa kuhusu alipo Mwita Yoba, kuwasiliana na kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja”