Meneja wa habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewachwa kinyua wazi baada ya Kutakiwa Kulipa bilioni kumi kwa kuichafulia jina Klabu ya Yanga. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni. Imebainika kuwa ametumiwa barua kutoka kwa Yanga ilikitaka alipe pesa hizo. Hili ni kutokana na makosa mawili ya kuzungumzia mkataba wa kiungo Pacome Zouzaua pamoja na tuhuma za ushirikina.
Kuhusu mchezaji Pacome Zouzaua Ahmed Ally amedaiwa kusema mchezaji huyo anamaliza mkandarasi yake ya Yanga na Simba wanatazama namna ya kumsajili na Kuna kauli za ukasi alizungumza ambazo zomeharibu brand.
Kauli ya Ahmed Ally kuhusu Pacome imesema kuwa Pacome Zouzaua amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika naye. Na kisha alidai kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni hasa kwa mashabiki na wasimamizi wa Klabu ya Yanga.
Aidha kuhusu tuhuma za uchawi Ahmed Ally ametakiwa kuthibitibisha namma gani Yanga ni wachawi kwa namna hawajawahi kupewa adhabu yoyote na bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuhusu uchawi. Kwa hivyo Yanga yamtaka aombe msamaha au atoe fidia ya shilingi bilioni kumi za Tanzania.
Asante kwa kusoma taarifa hii, unaweza kutoa maoni yako ili kuboresha uandishi wetu.