Aina za ndoto na maana zake, baadhi ya ndoto na maana zake




Hii itakuongezea maarifa, ukiota ujue nini ulichokiota, na maana yake, na namna utakavyoingia kwenye maombi juu ya hiyo ndoto.

1.WANYAMA:Kuota unakimbizwa na wanyama wakali inaasshiria mashambulizi ya kipepo,yaaani nguvu za giza zimejizatiti dhidi ya maish yako.

2. DAMU:Kuota/kuona damu kunaonesha kuna hatari mbele.Inaashiria kifo na ajali.Kwa mama mjamzito huashiria kuharibu mimba.

3. .NYUKI:Kujiona au kumuona mtu amezingirwa na nyuki ni ishara ya shambulizi la kiroho na kutofanikiwa kimaisha.

4. KUOGA:Inaonesha/inaashiria utakaso wa rohoni(utakatifu).

5. BIBLIA:Kuipoteza biblia yako inaashiria kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.

6. PAKA:Kuota paka ndotoni huashiria kuwa wachawi wanafuatilia maisha yako.

7. KUIBIWA TAJI:Inaonyesha kupoteza umaarufu na kurudi nyuma .pia inaweza kuashiria kushushwa cheo au wadhifa ofisini au katika nafasi yako kiuchumi au kisiasa.

8. .MLANGO ULIOFUNGWA:Unapo ota mlango wa ofisini kwako umefungwa dhidi yako inaashiria kupoteza kibali au kufukuzwa kazi.kama ni mlango wa biashara yako inamaanisha kunahatari ambayo itaua biashara yako.

9. JENEZA:Inaonesha kuwa roho ya mauti (kifo)inafuatiria maisha yako au umpendaye (rafiki wa karibu)

10. AGANO:Kufanya agano/kuingia kwanye agano na mtu yeyote ndotoni ni kifungo cha kiroho.

11. .MSALABANI:Inaashilia mzigo mkubwa na shida /taabu.

12. GIZA:Inaashiria kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.Iinaashiria kuzolota kiroho.

13. DENI:Kukupa ndotoni au kudaiwa kuashiria kudorora kiuchumi kiasi cha kuonyesha dalili zote za kufilisika.

14. .MBWA:Kucheza au kumbeba mbwa kunaashiria roho chafu (uovu) hasa wa usherati (uzinzi)

15. NDGU ALIYEKUFA:Kuota cha ndugu inaashiria uwepo wa mzimu wa familia.Uwe mwangalifu na ujumbe unaoweza kuonekana kama unapata taarifa muhimu lakini mungu hatumii njia za kipepo kusema na watoto wake SOMA 2WAKORINTHO 11:14 NA MHUBIRI 3:21.

16. KUNYWA POMBE:Kuota unakunywa pombe inaashiria kupenda ya dunia

17. ALAMA ZA KIPEPO:Unapoumizwa ndotoni au unapoamka na kukutwa alama mwilini mwako inaashiria magereza ya kiroho na kutumikishwa na mapepo.

18. PUNDA:Inaashiria ugumu wa mateso au shida katika maisha.

19. MITIHANI:Unaashiria majaribu na hali,kipindi kigumu.

20. KUPAA:Inaashiria kutawaliwa na wachawi,shambulizi la kiroho yaani kwamba huenda utachanganyikiwa.

21. KUVUA SAMAKI:Kuvua samaki inaashiria kuhubiri injili ya wokovu(soul winning)kama ilivyo katika biblia.

22. MOTO:Inaashiria kupoteza na majanga.

23. MAUA:Kupokea maua kutoka jinsi nyingine (kwa ambao hawajaoa au kuolewa)inaashiria kuwa mwenzi wako huenda atakujakuwa huyo huyo kwa maisha yako.

24. KUPIGWA RISASI(KUJERUHIWA):Inaonyesha udhaifu wa kiroho,shambulizina maadui wamejipanga kuharibu maisha yako.

25. KUPIGWA RISASI (ISIKUJERUHI):Inaonyesha ulinzi waakiungu na ushindi juu ya adui zako.

26. KUVUNA:Unapoota unavuna viazi,mihogo n.k.inaashiria Baraka za Mungu.

27. ASALI:Inaashiria Afya na mafanikio maishani mwako.

28. NYUMBA TUPU:Inaashiria hili ngumu na umaskini.

29. KUJIFICHA:Inaashiria maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa Mungu.

30. SAFARI:Unapoona na kujiona /kuona upo kwenye safari isiyokuwa na mwisho(kikomo)ina maanisha
unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza-poteza muda na nguvu.Hakutakuwa na matunda.

31. KUPOTEZA FUNGUO:Unapopoteza ufunguo wako ndotoni,inaashiria mlango wa Baraka zako
utafungwa.Inaweza hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango chanya,matarijio na matumaini yako kuhusu mafanikio.

32. FUNGUONYINGI:Unapoota na kukuta au kugundua umeshika funguo nyingi,inaashiria Baraka za fursa nyingi zinakusubiri maishani mwako.

33. KUPOTEZA PESA AU MALI: Inaashiria mambo mabaya au wezi wanaweza kuiba pesa au vitu vyako.Inaweza kumaanisha unataka kufanya biashara isiyo sahihi au kuangukia kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.

34. MZIGO: Kubeba mzigo inaashiria hili mbaya katika mateso na umasikini.

35. PESA: Unapoota mtu anakupa msaada au akukupa pesa bure,inaashiria kibali au neema maalumu na mpenyo wa kipesa mbele yako.

36. .MOCHWARI: Inaonyesha/inaashiria mauti inakufuatilia/ imekuzunguka wewe au mtu uliye muona kwenye hiyo ndoto.

37. UKICHAA: Unapoota umekuwa kichaa ndotoni,inamanisha shetani anataka kusababisha mvurugano katika maisha yako.Inamaanisha shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.unapoota unacheza na vichaa au watu wenye ukichaa pia inaashiria shambulizi la kiroho ili kukusambaratishia amani na utulivu.

38. WAHUNI: Unapoota umekimbizwa/umefukuzwa na wahuni,inaashiria nguvu za giza na wachawi wanajaribu kukuharibu(kukuua).

39. RUNGU: Niishara ya nguvu,pia inaashiria ukakamaavu kiroho na ulinzi wa kiungu.

40. NDOA: Unapoona unafunga ndoa na mtu asiyemjua,inaweza kuashiria mume/mke wa kipepo (kama ni mtu unayemjua lakini ameao/ameolewa,ni ishara ya kufanya kosa kubwa/hatari katika ndoa.Kama ni mtu unayemjua vizuri na wote mko na vijana na kama huna tama za mwili kwake (naye)hiyo inaweza kuwa ishara ya mwenzi wa maisha.

41. MIMBA KUTOKA/KUHARIBIKA:Kama mwanake mjamzito ,umeota mimba imetoka/imeharibika,usilichuklie kirahisi,pasipo kuangalia ni nani aliyesababisha hilo,kwani linaweza kutokea kiuhalisia.

42. UCHI/KUVUA NGUO:Inaashiria aibu au fedheha.

43. SIMBA:Kama katika ndoto yako umeshambuliwa na simba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.

44. BUNDI:Kuona bundi ndotoni inaashiria ubaya.ni taarifa kwamba kitu kibaya kitatokea/kinakwenda kutokea.

45. MTU ANAKUFUKUZA/ANAKUKIMBIZA:Kama katika ndoto yako umeota mtu unayemjua amekukimbiza akitaka kukua, mtu huyo anaweza kuwa hana mawazo/makusudi mazuri juu yako.Hata hivyo katika nyakati zingine wachawi hutumia sura ya mtu yeyote kulaghai,ilimradi tu ayaweke maisha yako hatarini.

46. NGURUWE:Ukijiona unacheza na nguruwe au hata kuwaona nguruwe ,huo ni uchafu kiroho,uzembe na kutokuwa makini katika maisha ya kiroho.

47. SHIMO:Inaashiria shetani ana mipango mibaya dhidi yako ili akuharibu.

48. KUCHEZWA NANYOKA:Hiki ni kuashiria kwamba umefungwa/unatawaliwa na Yule nyoka shetani.

49. .KONOKONO:Inaashiria kudumaa na kuzuiliwa kwa (maendeleo)au kukua kwa mtu.

50. SHULE:Unapoota mara kwa mara kurudi shule kusoma au kuwa shuleni,inamanisha unahitaji (mafunzo)kupata/kupitia mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako au utumishi wako katika maisha.kurudi shule za chuni au madarasa inaashiria kudumaa,yaani badala au kupiga hutua mbele unaridi nyuma kimaendeleo.

51. NGONO.Kufanya mapenzi na mtu ambaye siyo mwenzi wako wa maisha ni njia ya kwanza inayothibisha kutawaliwa na tama ya mwili,pili inaweza kuwa msukumo wa pepo kama unaendelea kufanya mapenzi na mtu usiyemjua.Roho ya uzinzi imeshakutawala

52. .MAJOKA:Inaashiria imetawaliwa na roho za majini au umeigia/umeingizwa kwenye agano hilo la mapepo/majini ya pwani baharini au mtoni.

53. NYOTA:Inaashiria ukuu.

54. MOSHI:Inaashiria shutuma na majaribu.

55. .RADI:Kamakulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na mawe ngurumo na radi,inaashiria matatizo na kuchanganyikiwa siku za usoni.

56. .KIJIJI:Unapoota kijiji chako mara kwa mara wakati wewe unaishi mjini hali hiyo inaashiria kuwa laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.

57. .KUNGURU:Inaashiria kifo au mauti mbele yako.

58. PETE YA NDOA(1):Kama mwanandoa umeota unapoteza pete yako ya ndoa,inaweza kuonyesha/kuashiria unahitaji kuwamwangalifu sana (ndoa)pia inaashiria matatizo ya ndoa mbele yako.

59. .PETE YA NDOA(2)Kama umepewa pete ya harusi ukiwa kijana,inaashiria kuolewa hivi karibuni,pia inaweza kumaanisha mtu (mhusika)ni mwenzi wako wamaisha

60. .KUTEMBEA BILA VIATU:Inaashiria shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na hali ngumu (shida au taabu) .

61. CHAKULA; ukiota unakula chakula au nyama, maana yake, unafanya maagano kwenye ulimwengu wa roho, hasa mikataba ya kichawi

Vitu vingi vinaonyesha namna shetani anavyoweza kutumia mlango wa ndoto, kuyashika maisha yako. Hivyo baada ya kupata maarifa haya, omba juu ya kila kitu chakwako kilichoibiwa kwa njia ya ndoto kirudishwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad