Ajali Mbaya Yauwa Watu Saba Mkoani Kagera, Lori Laparamia Magari

Ajali Mbaya Yauwa Watu Saba Mkoani Kagera, Lori Laparamia Magari

 Watu saba wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kihanga Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera ikihusisha gari kubwa la mizigo aina ya Scania ambalo limeyagonga magari mengine mawili ya abiria yaliyokuwa yamesimama ambayo ni Hiace inayofanya safari zake kati ya Karagwe na Mutukula pamoja na Coaster inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Karagwe leo December 03,2024.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amesema “Chanzo ni uzembe wa Dereva wa Scania ambaye alikuja akiwa na mwendo mkali akayagonga magari haya mawili yaliyokuwa na abiria ambayo yalisimama yakiwa yanakaguliwa na Maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji kwenye barrier ya ukaguzi”


“Katika vifo hivyo saba kuna Wanawake wanne, Mwanaume mmoja na Watoto wawili, kwenye majeruhi kuna Wanaume wanne na Wanawake watano, chanzo ni uzembe wa Dereva, kama ingekuwa mfumo wa breki umefeli asingeumaliza mteremeko na kona zilizo karibu na eneo la ajali, pia kuna vibao vinaonesha simama ukaguliwe”


“Ni wazi baada ya kumaliza mteremko hakuchukua tahadhari za barabarani, chanzo ni uzembe tu kutochukua tahadhari, nitoe rai kwa Madereva hizi barabara sio zetu pekee yetu tunatumia na Watumiaji wengine, kulikuwa na haja gani ya Dereva kuja na speed aliyokuja nayo!?, ukiangalia madhara ya Hiace aliyoigonga ni ishara alikuwa speed kali sana, nasikia ametoroka haitomsaidia, ajisalimishe mwenyewe kabla hatujampata, tuna mkono mrefu hawezi kutukimbia akasalimika ajisalimishe”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad