Ali Kamwe: Siamini Kama Shaffih Dauda Anaweza Kuandika Andiko la Kipuuzi Namna Ile


Kwanza, siamini kama Lile andiko ni mawazo ya @shaffihdauda_tz .. kwa uzoefu wake kwenye Uandishi na Uongozi kwenye Football, siamini anaweza kutoka Public na kuandika ‘Upuuzi’ wa kiwango kile

Anaweza kuwa yule kijana wake. Na ni kwa sababu zake za ushabiki na presha anayopewa na viongozi wa Makolo kuwa ‘wanamlipa halafu hawaoni akiwapiga Yanga’

Lakini kama ni mawazo ya @shaffihdauda_tz mwenyewe Basi Lile Linaweza kuwa ni andiko la HOVYO zaidi kutoka kwake tangu nimjue

Ni andiko lililobeba ajenda ya Chuki lenye Lengo la uchonganishi

Unaulizia Haki ya Taarifa kwa Mwanachama? Hili Lilifanyika.

Taarifa ilitoka kuwa Moalin ameajiriwa YANGA na nafasi yake kuwa ni MKURUGENZI WA UFUNDI.

Baada ya Hapa, kinachofatia ni MAJUKUMU ya Moalin kwenye Nafasi hiyo. Hii haijawahi kuwa Taarifa ya Lazima kwa PUBLIC

Hili ni jambo la ndani ya TAASISI Na mwajiriwa. Itakapoona anafaa na ana uwezo wa kufanya jambo, Linawekwa kwenye majukumu yake as long as halina athari hasi kwenye Utendaji wa Taasisi

Jambo Baya zaidi ni kama YANGA wangevunja KANUNI, Lakini kama Unamuona MOALIN benchi na BODI YA LIGI imeridhia maana yake YANGA Wamezingatia KANUNI zote.

Huko mbali, kwanza MAJUKUMU ya MKURUGENZI WA UFUNDI ni yapi kiasi Mtu huyu akiwa na vigezo vya kuwa sehemu ya benchi Liwe kosa?

Au na siku Mimi MKUU WA IDARA YA HABARI mkiniona napiga picha uwanjani mtahoji imekuaje Wanachama hawajui kama Kamwe anapiga picha?

Mechi na Mashujaa, Kocha wa Makipa wa @yangasc alikuwa anaumwa na hakuwepo kabisa uwanjani Lakini Majukumu yake ikiwemo Warm Up ya Magolikipa ilifanywa na VIDEO ANALYST wetu

Kwanini Video Analyst alifanya Jukumu Lile? Majukumu Yake ya kazi ndani ya Yanga yaliowekwa na Uongozi kutoka na CV yake yalitosha kabisa

Nikuombe Kaka yangu @shaffihdauda_tz Una nafasi ya kuwaomba radhi Mashabiki wa Yanga kwa andiko Lile la Uchonganishi

Na kama ni andiko la huyo kijana wako, Mkanye. Wanayanga sio wajinga, wanamjua na sasa washajua Lengo lake ovu kwa Klabu yetu

Ada za Wanachama wa @yangasc ndio zimeleta hii 𝐆𝐔𝐒𝐀 𝐀𝐂𝐇𝐈𝐀 𝐓𝐖𝐄𝐍𝐃𝐄 𝐊𝐖𝐀𝐎 .. Na niwaombe Wananchi Tuendelee Kulipia ADA ZETU

Hii Milio mnayoanza kuisikia Sio kwa Bahati Mbaya
KISU KISHAFIKA KWENYE MFUPA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad