Askari wawili wa Jeshi la Polisi Wafariki DUNIA Wakijibishana Risasi na Jambazi Sugu

Askari wawili wa Jeshi la Polisi Wafariki DUNIA Wakijibishana Risasi na Jambazi Sugu


 Askari wawili wa Jeshi la Polisi wamepoteza maisha katika kijiji cha Msagali, wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma, wakati wa operesheni ya kumkamata mtuhumiwa wa unyang’anyi wa kutumia silaha.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP George Katabazi, tukio hilo limetokea majira ya saa saba usiku, Jumatano Desemba 18, 2024. Askari hao, D/CPL Jairo Boniphace Kalanda na PC Alfred John, walikuwa wakijaribu kumkamata mtuhumiwa Atanasio Malenda (30), mkulima na mkazi wa kijiji hicho, ambaye alihusishwa na tukio la kumjeruhi na kumpora Yohana Lameck kiasi cha shilingi milioni mbili.


Kamanda Katabazi amesema kuwa askari hao walifika nyumbani kwa mtuhumiwa wakiwa na mwenyekiti wa kijiji kwa ajili ya kumkamata. Hata hivyo, mtuhumiwa alitoka ndani akiwa na silaha na kuanza kuwashambulia, hali iliyosababisha mapambano ya risasi na kusababisha vifo vya askari hao wawili.


"Askari Polisi walipata taarifa kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akitafutwa yuko nyumbani kwake. Walifika na kusindikizwa na uongozi wa kijiji, lakini mtuhumiwa alitoka ndani na kuanza kuwashambulia, na katika majibizano hayo ndipo vifo hivyo vilipotokea," ilisema taarifa ya Kamanda Katabazi.


Aidha, Kamanda Katabazi amebainisha kuwa mtuhumiwa, Atanasio Malenda, naye alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kutokana na majeraha aliyoyapata katika mapambano hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad