Balaaa Jipya la Bacca Huko Yanga, Anaongoza Kwa Mabeki Kufunga Magoli, Akitaka Kiatu

Balaaa Jipya la Bacca Huko Yanga, Anaongoza Kwa Mabeki Kufunga Magoli, Akitaka Kiatu


BAADA ya kupachika mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Prisons uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam juzi, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, anaongoza kwa kufunga mabao mengi kwa upande wa mabeki wa ligi hiyo.

Bacca ambaye ni beki wa kati ya Yanga, alipachika mabao dakika ya 42 na 83 na kuongoza Yanga kuiadhibu Prisons, kwa ushindi wa mabao 4-0, sasa amefikisha magoli manne kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa anaowaongoza wenzake wanaocheza nafasi ya ulinzi kwa kufunga mabao mengi.

Mabao mengine mawili alifunga dhidi ya KenGold, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Septemba 25, mwaka huu na mabingwa hao watetezi wakishinda bao 1-0.

Oktoba 3, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, akichangia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba Jiji alifunga bao lingine.

Mabeki wanaofuatia ambao wamefunga mabao mawili mawili kila mmoja ni pamoja na Shomari Kapombe na Fondoh Che Malone wa Simba, Anthony Trabita (Singida Black Stars), Erasto Nyoni (Namungo) na Nicolaus Gyan wa Fountain Gate.

Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Kapombe, beki wa kulia, alifunga bao timu yake ikapata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, kabla ya hapo alipachika bao lake kwa kwanza Oktoba 25, mwaka huu, kwenye Uwanja wa KMC Complex, Simba ikicheza dhidi ya Namungo na kushinda magoli 3-0.

Che Malone ni beki wa kati, raia wa Cameroon, alifunga bao la kwanza alilifunga Agosti 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa KMC Complex wakati Simba ikiizamisha Tabora United mabao 3-0 huku lingine akipachika Oktoba 22, kwenye Uwanja wa Sokoine na Mnyama kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad