Baleke Akubali Yaishe Yanga Baada ya Kuwa Butu, Kutimkia Namungo

Mshambuliaji Baleke Akubali Yaishe Yanga, Kutimkia Namungo kwa Juma Mgunda


Baada ya kutupia bao moja akiwa na Yanga, mshambuliaji Jean Baleke inaelezwa kwa sasa anajiandaa kuondoka, huku akitajwa huenda akaibukia Namungo inayonolewa na Juma Mgunda.


Nyota huyo wa zamani wa Simba, alirejea nchini mwanzoni mwa msimu huu akitokea Libya alikokuwa anacheza kwa mkopo akitokea kwenye klabu yake ya TP Mazembe, lakini amekuwa hana namba katika kikosi cha kwanza kuanzia kwa kocha Miguel Gamondi hadi Sead Ramovic anayeinoa timu hiyo kwa sasa.

Taarifa za ndani ya Yanga zinasema kuwa straika huyo yupo mbioni kupigwa chini katika dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Disemba 15, huku Namungo ikitajwa kutaka huduma yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad