Mfanyabiashara mashuhuri wa Kitanzania, Edhah Abdallah, kupitia kampuni yake Amsons Industries (K) LTD, amefanikisha ununuzi wa asilimia 96.4 ya hisa milioni 362.96 za Bamburi Cement, kwa jumla ya KSh 23.2 bilioni (Zaidi ya Shilingi bilioni 424).
Hatua hii inafanya Amsons kuwa mmiliki mkuu wa kampuni hiyo ya saruji yenye hadhi kubwa katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wanahisa wa Bamburi Cement waliidhinisha uhamisho wa hisa milioni 212.73, zenye thamani ya KSh 13.83 bilioni (TZS bilioni 252.94), kwa Amsons Industries.
Hii ilikuwa ni nyongeza kwa hisa milioni 137.06 ambazo Amsons ilikuwa imenunua hapo awali, na kufanikisha ununuzi wa jumla ya hisa kwa KSh 22.74 bilioni (TZS bilioni 415.90), kila hisa ikiwa imeuzwa kwa KSh 65 (TZS 1188.81).
"Ununuzi huu ni sehemu ya mkakati wetu wa muda mrefu wa kupanua uzalishaji wa saruji maalum. Ushirikiano huu mpya unalenga kuleta manufaa kwa pande zote mbili," Amsons Group imeeleza katika taarifa yao kwa vyombo vya habari.
Hata hivyo, ununuzi huu ulikuwa na changamoto. Kwa mujibu wa ripoti ya Business Daily, Amsons ilikamilisha mkataba huu baada ya kampuni ya Savannah Cement kujiondoa kwenye zabuni yake.
Mwenyekiti wa Savannah, Benson Nduta, alikumbwa na kesi za kisheria zilizohusiana na tuhuma za udanganyifu, hali iliyosababisha kampuni yake kushindwa kuendeleza zabuni ya KSh 75 (TZS 1371.70) kwa kila hisa.
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (CMA) ya Kenya ilitoa idhini rasmi ya mauzo haya, ikisisitiza kuwa wanahisa waliopinga uamuzi huo wataendelea kumiliki hisa zao ndani ya Bamburi Cement.
Kwa mujibu wa sheria za masoko ya mitaji, CMA ilieleza kuwa mchakato wa Savannah Cement ulipungukiwa na sifa stahiki baada ya mwenyekiti wake kukabiliwa na changamoto za kisheria.
Tangazo la Amsons Group kuhusu nia yao ya kumiliki asilimia 100 ya hisa za Holcim ndani ya Bamburi Cement lilichochea ongezeko kubwa la thamani ya hisa za kampuni hiyo.
Mnamo Julai, hisa za Bamburi zilipanda kwa asilimia 28.33 katika Soko la Hisa la Nairobi (NSE), zikifunga biashara kwa KSh 57.75 (TZS 1056.21) kutoka KSh 49.60 (TZS 907.15) asubuhi ya siku hiyo.
Ongezeko hili liliimarisha utendaji wa kampuni hiyo, ambapo kwa mwaka uliopita hisa zake zilipa