DEMOKRASIA: Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe, ametangaza kuwa atagombea tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho, ikiwa ni baada ya kupita Saa 48 alizoahidi kuwa atatoa msimamo wake kuhusu hatma yake ya Jongozi ndani ya Chama
Kauli ya Mbowe inafuatia madai ya kuwepo mvutano ndani ya CHADEMA juu ya anayepaswa kuwania nafasi hiyo ambayo tayari imetangazwa kuwaniwa na Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu
Amesema hayo leo Desemba 21, 2024 wakati akiwa anazungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam. Ikumbukwe Mbowe ametumikia nafasi ya Uenyekiti wa #CHADEMA kwa takriban miaka 20