Bunge Lapitisha Sheria Watu Kusaidiwa Kufa

Bunge Lapitisha Sheria Watu Kusaidiwa Kufa


Bunge la Uingereza limepitisha Sheria inayoruhusu Watu kusaidiwa kufa ambayo inawalenga Wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya kufisha kama vile Saratani ambapo wataweza kuomba kukatisha maisha yao kwa msaada wa Wataalam wa afya.


Mswada huo umepitishwa na Wabunge wa kuchaguliwa katika Bunge la House Of Commons ambapo Wabunge 330 wamepiga kura ya NDIO dhidi ya Wabunge 275 walioupinga Mswada huo uliopigiwa Kampeni kwa muda mrefu kabla ya kupita.


Hatua hiyo itaifanya Uingereza kuwa mojawapo ya Nchi chache duniani zinazoruhusu Watu kusaidiwa kujiua kama Mswada huo utapitishwa na Bunge la House Of Lords ambalo ni Bunge la pili la Uingereza linalowajumuisha Wabunge Wateule kama vile Majaji, Waadhiri na Watu walioteuliwa kutokana na ufanishi wao.


Sheria hii itaruhusu Wagonjwa ambao wamepewa taarifa na Madaktari kama wamebakisha kipindi cha miezi sita ya kuishi kuchagua njia ya kumaliza maisha yao kwa hiari lakini lazima ithibitishwe na Madaktati wawili na Jaji wa Mahakama Kuu kwamba Mgonjwa husika ameamua kufanya uamuzi huo mwenyewe.


Uingereza itajiunga na Nchi kama vile Canada, New Zealand, Uhispania, na baadhi ya Majimbo ya Marekani kama Oregon na California, ambapo tayari Watu wanaruhusiwa kujiua kwa kusaidiwa baada ya kuthibitishwa kuwa hawawezi kuendelea na maisha.


Wafuasi wa Sheria hiyo wanasema itawasaidia Wagonjwa kuepuka mateso ya mwili na kupunguza mzigo wa Huduma, Hata hivyo tafiti zinaonyesha kuwa Idadi kubwa ya Wananchi wa Uingereza wanaunga mkono Sheria hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad