Chalamila Awaomba Polisi Kuvaa Uniform Pale Wanaenda Kukamata Mtuhumiwa


 Chalamila Awaomba Polisi Kuvaa Uniform Pale Wanaenda Kukamata Mtuhumiwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema wamekaa na Viongozi wa Jeshi la Polisi kuwaeleza kuwa pale inapofaa wavae uniform za Polisi ili wanapoenda kuwakamata Watu wafanye ukamataji rasmi usioleta taharuki lengo likiwa ni Polisi kujitenga na Watu wachache ambao sio Raia wema wanaotumia pingu na bunduki kufanya uhalifu na kupelekea lawama zote kuelekezwa Polisi.


Akiongea Jijini Dar es salaam, Chalamila amesema “Wapo baadhi ya Watu wanaweza kuwa na pingu wanaweza kuwa na bunduki wanaweza kuwa hata na nguo za Polisi lakini wakiwa sio Polisi, sio Wanajeshi, sio Watu wa Uhamiaji wala sio Chombo Cha Dola kwakua baadhi ya Watanzania wamekwishafahamu pingu inahusiana na Polisi basi hata Majambazi na Watu ambao hawana nina njema wanweza kutumia hata pingu kuonesha au kuwa na bunduki ili tu nyinyi muhitimishe kuwa waliofanya jambo hilo ni Polisi”


“Tumekwisha kaa na Viongozi wa Jeshi la Polisi kuwaeleza nao katika nyakati hizi wachafuzi wa Taifa letu na wao wanafanya struggle basi pale ambapo yafaa kuvaa uniform za Polisi wavae nao ili wafanye ukamataji rasmi ambao hautaleta taharuki kwa Watanzania, kwa kufanya namna hiyo Taifa letu litaendelea kuwa na amani na Taifa letu kamwe halitaingia katika mchafuko ambayo baadhi ya Watu wachache hupenda kufanya hivyo”


RC Chalamila ameyasema hayo wakati akizungumzia matukio yaliyotikisa Dar es salam ya utekaji na kuelekea sherehe za Christmas na mwaka mpya”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad