Hakuna asiekumbuka kilichotokea baada ya Simba kuongezewa dakika 7, mechi dhidi ya Cs Sfaxien.
Waarabu baada ya kupigwa kidude kimoko na Kibu Mkandaji, mechi imeisha wakafanya sana vurugu; Mixer kuvunja viti na kutaka kumpasua refa.
CAF wakasema aaaah nyie msitutanie? Hamna uhuru kiasi hicho.
The good news ni kwamba, waarabu Cs Sfaxien wamepewa adhabu mbili kwa mpigo.
Moja; Mechi zao mbili zifuatazo wakiwa nyumbani kwako; Cs Sfaxien vs Simba, na Cs Sfaxien vs Bravos zitachezwa bila mashabiki.
Mbili; Adhabu ya kulipa milioni 119 [ USD 50,000].
Kichapo walichezea, na adhabu wamepata, hasira zao wakamalizie uwanjani sasa.
Ama namna gani?