Diddy Mambo Yazidi Kuwa Mabaya Afunguliwa Keshi Nyingine Fidia Bilioni 36
Mwanamuziki na mfanayabiashara Diddy anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya unyanyasaji wa kijinsia, zikiwemo kesi za ubakaji na usafirishaji wa binadamu, zinazotajwa kuzidi 100.
LaTroya Grayson amemshtaki Diddy kwa kudai fidia ya dola milioni 15, akidai alidungwa dawa, kushambuliwa kijinsia, na kuibiwa kwenye sherehe ya Diddy mwaka 2006. LaTroya alisema alipoteza fahamu baada ya kunywa vinywaji kwenye sherehe na anachokumbuka ni kujikuta hospitalini bila nguo na pesa zake.
Pia, mwanamke mwingine, Jane Doe, anadai kuwa alibakwa na Diddy mwaka 1991 kwenye tukio la hisani kwenye chuo kimoja jijini New York.
Wakili wa Diddy amekanusha madai haya, akiyaita ya uongo na ya kupangwa kwa nia ya kujipatia pesa.