Donald Trump 'Nitakomesha Upuuzi wa Kubadili Jinsia"

Donald Trump 'Nitakomesha Upuuzi wa Kubadili Jinsia"


Rais Mteule wa Marekani Donald Trump ameahidi kukomesha kile alichokiita upuzi wa Watu wanaobadili jinsia zao, siku ya kwanza tu atakapoingia madarakani.


Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa kauli hiyo ameitoa wakati Warepublican wanaotarajiwa kudhibiti Mabunge yote mawili ya Marekani wakiendelea na juhudi zao za kupinga haki za Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTQ.


Trump amesema atasaini agizo la kiutendaji kukomesha ukeketaji wa Watoto na kuwaondoa Watu waliobadili jinsia zao jeshini na mashuleni.


Kiongozi huyo ameahidi pia kuwazuia Wanaume kushiriki michezo ya Wanawake na kuongeza kwamba itakuwa sera rasmi ya Marekani kuwepo kwa jinsia mbili pekee, Mwanaume na Mwanamke.


Suala la Watu waliobadili jinsia zao limezua mjadala mkubwa wa kisiasa huku Warepublican na Wademocrats wakionesha msimamo tofauti juu ya sera kama vile matibabu na aina ya vitabu vinavyoruhusiwa kwenye maktaba za umma au shule kuhusu maudhui ya mapenzi ya jinsia moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad