Elon Mask Ajifanya Maskini Kuwapima Wafanya kazi wa Benki



Tajiri namba moja Duniani na mmiliki wa Makampuni mbalimbali kama Space X na Tesla, Elon Musk hivi karibuni amezua gumzo baada ya kujifanya kama mtu maskini asiye na makazi akilenga kupima uwajibikaji katika makampuni, lakini pia kupima utoaji wa huduma kwa watu wa vipato tofauti.

Elon Musk ambaye mara zote amekuwa akihubiri kuhusu usawa na huruma kwa wengine, katika jaribio hilo alivaa mavazi machafu na kuweka ndevu pamoja na nywele nyingi kichwani kwake, na kufanya kuwa na muonekano wa mzee, huku akiigiza kama mtu mwenye hofu na baadaye aliingia katika benki moja kubwa huko Metropolitan.

Baada ya kuingia katika benki hiyo wafanyakazi walionekana kusita na kuogopa baada ya kumuona, huku walinzi wakianza kumuangalia kwa ukaribu zaidi, Elon alinyooka moja kwa moja kuelekea katika dawati la huduma kwa wateja na kwa utaratibu aliomba kufunguliwa akaunti ili aweke kiasi cha pesa alichokitunza.

Elon Musk alisema: ” Nilihisi wakiogopa, muonekano wangu uliamua kama ninastahili muda wao.” Jambo la kushangaza lilitokea baada ya meneja wa benki hiyo aliyeitwa Clara kuingilia mazungumzo na kumkalimu Elon Musk na kuanza kumuelezea aina za huduma zinazotolewa pamoja na ushauri wa kifedha.

Baada ya kupata huduma Elon Musk aliamua kujiweka wazi kwa kuondoa muonekano wa bandia aliokuwa nao na kuwaacha wafanyakazi na wateja wote wakishangaa, kisha Musk alimwagia sifa meneja wa benki hiyo kwa ukarimu aliouonyesha na kuomba kuonana na viongozi wa benki hiyo.

Elon Musk baada ya kukamilisha jaribio lake alisema kuwa “hii haikuwa kuhusu kumdhalilisha mtu yeyote, ilikuwa kuhusu kuanzisha mazungumzo, sote tuna upendeleo, lakini sote tuna uwezo wa kuushinda.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad