Eng Hersi na Mangungu Wamtaka Karia Aendelee Kuwa Rais wa TFF Muhula Ujao...


MANGUNGU, HERSI WAMPIGA MANDE KARIA.

Mande hiyo imetokea leo katika Mkutano mkuu wa uchaguzi wa TFF.

Bila kupepesa macho Mzee Mangungu alisema kuwa;

“Atakayechukua fomu ya kugombea urais wa TFF mwakani, atakuja kutueleza kuwa atafanya jambo gani kubwa ambalo wewe umeshindwa kulifanya, Lipi? Hawa wajumbe wa Kamati ya utendaji ndiyo twende kwenye uchaguzi ili kuongeza efficiency na uhuru mzuri lakini hili la Rais tulimalize, mkutano huu uamue, tuende mbele, uendelee kufanya kazi”

Lakini sio Mangungu, hata Rais wa Yanga Hersi Said alisema kuwa;

“Nipongeze wazo zuri la kaka yangu Mangungu, mimi binafsi naunga mkono kwa 100%”

Mande waliyopiga Mangungu na Hersi kwa Rais wa TFF, Wallace Karia ni katika kuchagiza kuwa mambo yasiwe mengi, Karia aaminiwe kuongoza tena shirikisho hilo.

Mdau una maoni gani juu ya hilo?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad