Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kuwa shabiki mmoja wa klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia ameumia kufuatia fujo zilizotokea katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Simba Sc dhidi ya CS Sfaxien.
Taarifa ya leo Desemba 15, 2024 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro J. Muliro imeeleza kwamba fuzo hizo zimesababishwa na mashabiki wa CS Sfaxien baada ya kutoridhika na maamuzi ya refa wa mchezo huo kuchezesha mechi hiyo kwa zaidi ya dakika saba ambazo aliziongeza kama dakika za nyongeza jambo lililopelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi.
Wachezaji wa ndani ya uwanja na benchi la ufundi la timu ya CS SFAXIEN walikasirika, wakamfuata mwamuzi wa mchezo na kuanza kufanya vitendo vya kumshambulia huku viti vya rangi ya blue 156 na Orange 100 viling'olewa na mashabiki hao.
Jeshi la Polisi limesema shabiki huyo aliyeumia amepatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa na kubainisha kuwa litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria na soka kuona hatua za kuchukua dhidi ya vitendo hivyo ambavyo havikubaliki.
#KitengeUpdates