Mzee Japhet Munisi ambaye ni baba mkwe wa marehemu Ulomi amethibitisha taarifa hizi za kusikitisha.
Ikumbukwe kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro J Muliro mnamo Disemba 14, 2024 alitoa taarifa kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kupotea kwa Daisle Simon Ulomi, ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini kwake Disemba 11.
Muliro alisema kuwa siku hiyo Ulomi alionekana akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni majira ya saa 6:00 mchana kuelekea Mbagala, Bandari kavu alikodai anaenda kukagua ‘container’ la bidhaa zake baada yakuitwa na watu aliodai ndiyo waliokuwa wanashughulika na kutoa kontena hilo bandarini na alikuwa akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe.