Hatimaye Monalisa Ahitimu Chuo Kikuu, Alichekwa Kisa Umri Kuenda

Hatimaye Monalisa Ahitimu Chuo Kikuu, Alichekwa Kisa Umri Kuenda

Monalisa, ameonyesha mfano wa kuigwa kwawanaotakakufanikisha ndoto zao za kurudi shule wakiwa na umri mkubwa. Muigizaji huyo amefanikiwa kujipatia shahada katika fani ya Biashara na Usimamizi wa Miradi. Kupitia instagram, @Monalisatz alifweka wazi changamoto alizokutana nazo, ikiwemo kudharauliwa na kubezwa kwa kuamua kurudi darasani akiwa na umri mkubwa zaidi ukilinganisha na wanafunzi wenzake.

Hata hivyo, juhudi na uvumilivu wake zimemletea matokeo bora, kwani alitunukiwa cheti cha 'Best Performing Graduant' huku akihitimisha masomo yake kwa kiwango cha juu. "Huu ni ushuhuda wa uvumilivu, ujasiri na uthubutu," alieleza Monalisa huku akiwahimiza watu kuwa hakuna umri wa kuchelewa kufanikisha ndoto.

Monalisa amethibitisha kuwa hatua yake ya kurudi shuleni ni mwanzo wa mambo makubwa zaidi yanayokuja, huku akisisitiza kuwa hakuna kurudi nyuma. Amehimiza jamii kuwa na uthubutu wa kujaribu, kwani mafanikio yanawezekana kwa yeyote aliye na dhamira thabiti.

Hongera Monalisa kwa kuvunja vizuizi na kuonyesha kuwa ndoto hazifi kwa sababu ya umri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad