Huu Hapa Uamuzi wa TFF Sakata la Mchezaji Lawi Kuhusu Kucheza Simba au Yanga

Huu Hapa Uamuzi wa TFF Sakata la Mchezaji Lawi Kuhusu Kucheza Simba au Yanga


LILE sakata linalomhusu beki wa Coastal Union dhidi ya klabu ya Simba limechukua sura nyingine baada ya leo Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukutana jijini Dar es Salaam.

Simba iliamua kurejea TFF kutokana na kusikia watani wao wa jadi, Yanga wameanza kumnyemelea beki huyo aliyetambulishwa na Wekundu hao katikati ya mwaka huu, lakini akaishia kutimia Ubelgiji alipoenda kufanyiwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya KAA Gent.

Ipo hivi. Klabu za Simba na Coastal Union zimerudishwa tena mezani kujadiliana na kulimazika sakata la beki wa kati, Lameck Lawi anayegombewa na pande hizo mbili tangu dirisha kubwa la usajili nchini.

Lawi anayeitumikia Coastal, alitambulishwa na Simba Juni 22, mwaka huu kama mchezaji wa kwanza kusajili, lakini wagosi waliibuka na kusema dili la mauziano ya mchezaji huyo lilishakufa kutokana na Wekundu kupeleka fedha kwa mafungu.

Hata hivyo, Simba haikukubali na kukimbilia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ambayo ilizitaka pande hizo mbili zikae chini na kumalizana zenyewe, wakati huo Lawi alishapaa zake kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya KAA Gent ya Ubelgiji.

Baada ya beki huyo kukwama kujiunga na timu hiyo, alirejea na moja kwa moja kuendelea kuitumikia Coastala huku Simba ikifanya chapu kumvuta Abdulrazak Hamza kutoka Afrika Kusini kuziba nafasi hiyo iliyokuwa imilikiwe na Lawi, lakini juzi kati baada ya kusikia tetesi kwamba Yanga inamnyemlea ilirudi tena TFF.

Kitendo hicho kimefufua upya kesi ya vigogo hao ambapo leo imesikilizwa huku Simba ikidai ina uhalali wa nyota huyo kutokana na makubaliano ya awali.

Katika kesi hiyo ambayo imesikilizwa leo kuanzia saa nne na wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kupitia kwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Said Soud, imeachia timu hizo kukaa mezani zenyewe ili zimalizane juu ya suala hilo.

Viongozi wa Simba na Coastal Union waliohudhuria kesi hiyo kwa ajili ya shauri hilo, walilsema kwamba uamuzi umefikiwa na wanaenda kujadiliana ili wayamalize.

“Kamati imetusikiliza na kututaka tukakae chini wenyewe ili tumalizane, naamini suala hili litafikia muafaka na kuendelea na mambo mengine,” amesema mmoja wa viongozi wa Coastal Union ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutokana na kutopewa ruhusa ya kuongelea uamuzi wa kamati.

Mbali na sakata hilo, kesi nyingine zikiendelea kusikilizwa ni aliyekuwa Kocha wa Geita Gold, Denis Kitambi inayeelezwa anaidai timu hiyo fedha na haijamlipa baada ya kuondoka kisha kujiunga na Singida Black Stars ambayo pia ameachana nayo hivi karibuni.

Kesi nyingine ambayo ilikuwa inasikilizwa ni ya mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha Mnunka aliyeondoka kambini bila ridhaa ya viongozi wa kikosi hicho cha Msimbazi, huku ikielezwa hataki tena kuichezea timu hiyo msimu huu licha ya mkataba aliokuwa nao.

Mbali na hilo, ila zipo kesi za nyota wa Tabora United wakiongozwa na nahodha wa kikosi hicho, Said Mbatty ambaye inaelezwa alisimamishwa kutoichezea timu hiyo tangu msimu huu umeanza baada ya kudai stahiki zake za fedha anazowadai viongozi.

Hata hivyo, kamati hiyo inasubiriwa kutangaza kilichotokea kwa kesi zote mara baada ya kumalizika kuzipitia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad