Chini ya makocha wawili waliopita (Nabi & Gamond) Yanga walicheza mpira wa pasi nyingi,Yanga walikuwa na utaratibu wa kuwatongoza wapinzani kwa pasi nyingi kabla ya kufunga magoli (TIP TAP FOOTBALL) ila chini ya Ramovic tunashuhudia pira “Gegen-Pressing” au kwa kizungu tunasema “Counter-pressing).
-Yanga ya Ramovic haitaki pasi 10 kufika kwenye lango la mpinzani,badala yake inahitaji pasi tatu hadi nne kufika kwako na kukufunga✍️
-Yanga ya Ramovic haitaki back-pass wala Sideway pass,mchezaji akiiba mpira ni kwenda mbele Yanga wako direct sana✍️
-Yanga ya Ramovic haipigi cross nyingi za juu,badala yake mashambulizi mengi yanatokea pembeni kwa fullbacks na wingers kisha zinapigwa V-pass kwenye 12 na viungo washambuliaji wanafunga…..rejea magoli mawili ya Pacome leo✍️
JINSI GANI YANGA WANAWEKA MTEGO KABLA YA KUFANYA PRESSING?
Mara nyingi tumezoea kuona mstari wa kwanza wa namba 9 na 10 ukianzisha pressing kwa walinzi wa timu pinzani,ila Yanga ya Ramovic,inasubiri wapinzani wafike kati kati ya uwanja kisha viungo wazuiaji (Aucho na Muda) wanaweka pressure kwa mchezaji mwenye mpira huku walinzi wa kati (Job na Bacca) wakisogea kati kati ya uwanja kukata passing option…..baada ya kuiba mpira unapigwa pembeni kwa mawinga na fullbacks kisha shambulizi linaanzia hapo✍️
Ndugu zangu huu mpira wa Yanga una magoli mengi ya “Turnovers” wapinzani wanafanyishwa makosa mengi na kuhadhibiwa.
FT Yanga 5-0 Fountain Gate.