Akili yake ime’balance na mwili. Nguvu za kutosha, mwendo anao.
Anachojua zaidi yeye ni kucheza ndani ya boksi la mpinzani.
Weka pasi ya chini
Weka pasi ya juu
Yeye hana noma, atazifanyia kazi pasi zote.
Wakati anatoka Kenya alimaliza ligi akiwa top scorer na bao 27
Alivyokuja Bongo msimu wake wa kwanza ligi ilikua ngumu sana kwake. Na yeye mwenyewe alisema kuwa;
“Nilipokuja Tanzania mara ya kwanza, niliwaza kuwa ligi itakua ya kawaida. Lakini baada ya kuanza kucheza, nilitamani kukimbia nirudi nyumbani [Kenya]. Ile miezi 6 ya kwanza ilikua migumu sana kwangu, ila ni ligi iliyonijenga na kunikuza sana”
Ladies and Gentleman, namtambulisha kwenu kiongozi wa mabao mpaka sasa NBC PREMIER LEAGUE, Elvis Rupia. Bao 07 kambani, na wala haringi.