Jay Z Atuhumiwa Kumbaka Mtoto wa Miaka 13 Mwaka 200


MAREKANI: Rapa Mkongwe na Mfanyabiashara Shawn Carter maarufu kama JAY-Z ameingia kwenye kashfa za Ubakaji baada ya kushtakiwa kwa madai ya kumpa #DawaZaKulevya mtoto mwenye miaka 13 na kumbaka mwaka 2000, kesi inayomhusisha pia Rapa Sean Combs ‘Diddy’

Mlalamikaji (Utambulisho wake umefichwa) amedai alifanyiwa kitendo hicho baada ya utoaji Tuzo za Muziki za Video za MTV ambapo alichukuliwa na Dereva wa Diddy na kupelekwa kwenye sherehe zilizofanyika nyumbani kwa Diddy ambapo alitakiwa kusaini hati ya makubaliano ya kutofichua atakachoona au kushiriki ndani ya jumba hilo (NDA)

Awali, kesi ilimhusu Diddy pekee lakini imefunguliwa upya na kumwongeza JAY-Z ambaye ametoa taarifa ya kukana tuhuma hizo na kueleza kuwa Mwanasheria aliyefungua kesi hizo za madai analenga kujipatia Fedha na kumharibia heshima yake mbele ya jamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad