Jeshi la Polisi Laanza Uchunguzi Mfanyakazi wa Ndani Aliyejinyonga Kwa Kamba




Jeshi la polisi nchini Tanzania limetoa taarifa muhimu kuhusu dada wa kazi Aliyekutwa amejinyonga. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, mfanyakazi wa ndani aliyefahamika kama Modesta (17) amefariki dunia baada ya kujinyonga Desemba 10, mwaka huu, mtaa wa Zanzibar katika manisipaa ya Musoma mkoani Mara. Kamanda wa Polisi mkoani humo, Pius Lutoma amesema mwili wa binti huyo ulikutwa umening'inia kwenye chumba alimokuwa akilala binti huyo enzi za uhai wake, huku chanzo cha tukio hilo kinahusishwa na msongo wa mawazo. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni.

Kwa hivyo jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi wa tukio la kujinyonga mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa ndani. Tukio hilo lilitendeka Desemba 10, 2024 saa 5:40 katika eneo la Zanzibar Musoma

Jeshi la polisi nchini Tanzania pia limeelezea kuwa alijinyonga kwa kutumia kamba ya kufungia mbuzi huku uchunguzi wa awali ukionyesha sababu ilikuwa ni msongo wa mawazo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad