Jeshi la Polisi Lafunguka Kuhusu Kutekwa Kwa Abdul Nondo wa ACT Wazalendo

Jeshi la Polisi  Lafunguka Kuhusu Kutekwa Kwa Abdul Nondo wa ACT Wazalendo


Jeshi la Polisi limesema leo December 01,2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es salaam kuna Mtu mmoja Mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na Watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Landcruiser rangi nyeupe na kwamba ilielezwa na Mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baaadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mara tu baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada”

Taarifa ya Polisi inakuja saa chache baada ya Chama cha ACT Wazalendo kusema Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Abdul Omar Nondo ametekwa na Watu wasiojulikana asubuhi hii leo katika stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi Luis Jijini Dar es salaam wakati akitokea Mkoani Kigoma alikokuwa sehemu ya Viongozi wa Kitaifa walioongoza kampeni kwenye Mikoa ya Magharibi mwa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi ACT Wazalendo, Mbarala Maharagande imesema Nondo aliwasili stendi ya Magufuli iliyopo eneo la Mbezi kwa usafiri wa basi la Saratoga lenye namba za usajili T 221 DKB na kwamba Mashuhuda wa tukio wanasema kuwa kulikuwa na purukushani katika utekaji wa Nondo iliyosababisha begi lake dogo la nguo na pingu iliyobebwa na mmoja wa Watekaji kudondoka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad